Mshambuliaji Yacouba Songne ameahidi kuwapa furaha mashabiki wa Yanga baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki nne
Tangu akosekane kikosini pamoja na Saido Ntibazonkiza, Yanga inakabiliwa na changamoto ya kufunga mabao licha ya kutengeneza nafasi nyingi
Yacouba amefunga mabao manne na kutoa pasi nne za mabao katika ligi msimu huu
Nyota huyo raia wa Burkina Faso, amesema amerejea kuipambania Yanga kuhakikisha wanapata matokeo mahali popote
"Nitahakikisha naipambania timu yangu Yanga kupata matokeo popote inapokwenda na Uwanja wowote na niko timamu kuwavaa Coastal Union"
"Waambie wanachama, wapenzi na Mashabiki wajitokeze ili kutupa hamasa bila hofu ya aina yeyote tuchukue alama tatu muhimu hapa Tanga," amesema Yacouba
mchezo dhidi ya Coastal Union unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka jijini Tanga na nchi nzima
Yanga inasaka ushindi wake wa kwanza katika uwanja wa Mkwakwani wakishindwa kufanya hivyo tangu mwaka 2015