Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema hawafikirii kuachana na kocha Cedric Kaze kwa kuwa wamemleta kwa mpango wa muda mrefu
Aidha Hersi amewataka Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wasikubali kuingizwa kwenye mijadala ambayo inalenga kuwavuruga
"Sisi hatufikirii kuachana na Mwalimu Kaze kwa kuwa tumemleta kwa mpango wa muda mrefu"
"Viongozi , Wadhamini kila mmoja ana imani kubwa na Kaze. Wakati mwingine kuna mambo yanaweza kutokea ambayo yako nje ya uwezo wake. Kwa muda aliokaa nasi ametengeneza timu imara, kazi hiyo anaendelea nayo na tunaimani atatufikisha pale ambapo kila mmoja wetu anatamani tufike"
"Nawaomba wapenzi, wanachama na mashabiki wetu wasikubali kuingizwa kwenye mijadala ambayo haina malengo mazuri kwa klabu. Yanga bado haijafanya vibaya, tumepata matokeo ya sare tu, hatujapoteza mchezo wowote msimu huu. Tuko imara na kwa umoja wetu tutaweza kufikia malengo tuliyojiwekea ambayo ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu na FA," amesema Hersi
Yanga iko jijini Tanga ambapo kesho Alhamisi watashuka katika uwanja wa Mkwakwani kuikabili Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom