Alhamisi ya Machi 4, Yanga itashuka dimbani kuvaana na Coastal Union kwenye mchezo wa VPL ndani ya dimba la Mkwakwani Tanga
Mshambuliaji Yacouba Songne ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri kwenda jijini Tanga
Mpaka sasa Yacouba ameshatikisa nyavu mara nne kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na kutoa pasi za mabao manne
Bao lake la kwanza alifunga kwenye mtanange uliopigwa dimbani Benjamin Mkapa dhidi Coastal Union, Oktoba 3, 2020, akipokea pasi kutoka kwa Mukoko Tomombe
Goli lake la nne alifunga kwenye mchezo dhidi ya Ihefu SC, Disemba 23, 2020, akipokea pasi kutoka kwa Saidi Ntibazonkiza
Mpaka sasa mchezaji huyo amecheza dakika 858, kuitumikia Yanga kwenye michezo yake Ligi Kuu Tanzania Bara
Alhamisi watakuwa ugenini huko 'waja leo warudi leo’ jijini Tanga. Bila shaka kama atapewa nafasi na Kocha Cedric Kaze, anaweza kuendeleza pale alipoishia katika mchezo wa kwanza