Zahera awashangaa wanaomponda Sarpong

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Mar 2021
Zahera awashangaa wanaomponda Sarpong

Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amemtaja mshambuliaji Michael Sarpong kuwa miongoni mwa wachezaji wazuri ambao klabu ya Yanga imewasajili

Zahera ametofautiana na wale wanaomponda mshambuliaji huyo anayekabiliwa na ukame wa mabao

Mcongoman huyo amesema anaamini benchi la ufundi la Yanga halijapata namna sahihi ya kumtumia mshambuliaji huyo ili aweze kuwa na faida

"Mimi kama ningekuwa Yanga ningeletewa Sarpong ningemsajili haraka sana, yule ni mshambuliaji hatari, watu hawajui kabisa ubora wake ndio maana wanalaumu," Zahera alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Kuna namna ya kumfanya mshambuliaji wa aina ile awe anafunga, nadhani hapo ndipo penye tatizo. Benchi la ufundi ndilo lenye jukumu la kumjenga kupitia video zake za nyuma wanaweza kubaini mapungufu yake na kumsaidia kuanzia hapo"

"Sarpong ni mchezaji anayejituma sana uwanjani. Walinzi huhofia wachezaji aina yake. Angalia akiwa na mpira hakuna beki anayeweza kuwa na raha, kila wakati beki anaona yuko hatarini. Baada ya hapo ni kazi ya makocha kumjenga kimbinu ili aweze kuwa na madhara zaidi," alisema Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amewahi kunukuliwa akisema kuwa anaridhika na kazi anayoifanya Sarpong uwanjani licha ya kuwa wakati mwingine hafungi

Kaze alisema kazi ya mshambuliaji sio kufunga tu, pia anaweza kuwa msaada kwa wenzake kufunga

Sarpong amefunga mabao manne kwenye ligi msimu huu na kutoa pasi mbili za mabao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’