Kaze apania ushindi Tanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Mar 2021
Kaze apania ushindi Tanga

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa kombe la Shirikisho, Yanga inarudi kwenye mikiki mikiki ya ligi kuu wakisafiri mkaoni Tanga kuifuata Coastal Union

Vinara hao wa ligi kuu watashuka uwanja wa Mkwakwani siku ya Alhamisi, March 04 kuwakabili Coastal Union

Yanga itashuka dimbani katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Cedric Kaze dhidi ya Coastal Union kwani wakati anajiunga na Yanga mwezi Oktoba mwaka jana, tayari wananchi walikuwa wameshachukua alama zao tatu kwa Coastal Union katika mchezo ambao Carlinhos, Haruna Niyonzima na Yacouba Songne waliingia kambani

Kaze amesema wanahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ndani ya kampeni yao ya kushinda ubingwa msimu huu

Hata hivyo dimba la Mkwakwani mara nyingi limekuwa sio rafiki kwa Yanga kupata matokeo

Katika misimu miwili iliyopita, Yanga imeshindwa kuondoka na alama zote tatu ingawa pia hawakupoteza mchezo

"Tumefuzu kwenye round ya inayofuata FA Cup, nguvu zetu zote tumezielekeza kwenye mchezo wetu wa ligi kule Tanga dhidi ya Coastal Union tarehe 4 March," alisema Kaze baada ya ushindi dhidi ya Ken Gold juzi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’