Tanzania Prisons wamepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sahare All Stars katika mchezo wa raundi ya nne ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Prisons sasa wanakwenda kukutana na Yanga katika mchezo wa hatua ya 16 utakaopigwa kule Rukwa
Huo utakuwa mchezo wa tatu baina ya timu hizo msimu huu, mechi mbili za ligi kuu zikimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Mshindi lazima apatikane katika mchezo huo, dakika 90 zikimalizika kwa sare, changamoto ya mikwaju ya penati itatumika kuipata timu itakayotinga robo fainali
ADVERTISE HERE