Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewataka Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuiunga mkono timu yao wakati benchi la ufundi likiendelea kuimarisha timu ili iweze kufikia katika kiwango ambacho kila mmoja anatamani
Nugaz amesema anaamini wachezaji wanastahili kupewa muda kwani kujenga kikosi chenye ushindani sio jambo la siku moja
"Naamini kwenye muda kwa Kikosi chetu kuweza kukaa sawa na kupata matokeo stahiki zaidi kama ambavyo wanachama, wapenzi na Mashabiki wanatamani yapatikane"
"Kujenga kikosi sio jambo jepesi ni mchakato endelevu ambao unahitaji muda zaidi kuliko kitu chochote"
"Kwahiyo ni lazima wanachama, wapenzi na Mashabiki tuendelee Kuwapa muda Wachezaji wetu ili waendelee kupata upatano wa kitimu"
"Tuwe na Subra na uvumilivu kwa ushindi mwembamba tunaopata. Kikubwa Mwalimu na benchi la ufundi wanaona mwenendo wa Kikosi na watayafanyia kazi mapungufu madogo madogo yanayojitokeza," amesema Nugaz