Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa mazungumzo ya kumuuza winga wake Simon Msuva kwa klabu Difaa El Shadida yamekwenda vizuri na sasa limebaki swala maslahi binafsi ya mchezaji.
Akizungumza baada ya kumtambulisha mshambuliaji mpya wa Yanga Ibrahim Ajib leo, Mkwassa amesema Yanga haina pingamizi, Msuva anaweza kuondoka wakati wowote kama maswala hayo yatakamilika.
"Tumezungumza na hiyo timu ya Morocco na tumefikia makubaliano. Swala lililobaki ni maslahi binafsi ya mchezaji. Sisi hatuna tatizo kwa Msuva kuondoka kama kila kitu kitakamilishwa" ameeleza.
Msuva yuko kwenye timu ya taifa inayoshiriki michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini ikiwa imetinga hatua ya nusu fainali.
Stars leo inashuka dimbani kuchuana na Zambia katika mchezo wa nusu fainali.

ADVERTISE HERE