Carlinhos aomba radhi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Feb 2021
Carlinhos aomba radhi Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Carlos Carlinhos amewaomba radhi wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki kufuatia kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ken Gold uliopigwa uwanja wa Uhuru leo

Katika mchezo huo ambao Yanga iliondoka na ushindi wa bao 1-0, Carlinhos alifanya kosa la kumpiga ngumi mlinzi wa Ken Gold na hivyo kupelekea kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja

Kadi hiyo itamfanya akose mechi tatu za ligi au FA kwani kanuni za uendeshaji wa michuano ya FA ni zilezile za uendeshaji wa ligi kuu

"Nawaomba radhi mashabiki, wachezaji, benchi la ufundi na uongozi kwa kadi nyekundu niliyopata leo. Naahidi nitarejea nikiwa makini na imara baada ya kumaliza adhabu yangu, nitahakikisha naisaidia timu kufikia malengo yake," alisema Carlinhos

Matukio kama haya huwatokea wachezaji wengi hasa pale damu inapokuwa imechemka uwanjani

Bila shaka Carlinhos atakuwa amepata funzo kuwa wakati mwingine hapaswi kukubali kutolewa mchezoni na kufanya matukio ambayo yanaigharimu timu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’