Yanga imefuzu hatua ya 16 bora michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Ken Gold bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Bao pekee la Yanga lilifungwa na Fiston Abdulrazak katika dakika ya 42 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Ken Gold kuuwana mpira ndani ya eneo la hatari
Kwa muda mwingi Yanga ilitawala mchezo katika vipindi vyote lakini bado changamoto ilionekana katika kutumia nafasi kufunga mabao
Katika mchezo huo Kocha Cedric Kaze alifanya mabadiliko ya kikosi akiwapa mapumziko baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza



Katika dakika ya 81 kiungo Carlos Carlinhos alifanya kosa la kizembe lililopelekea azawadiwe kadi nyekundu ya moja kwa moja baada kumpiga ngumi mlinzi wa Ken Gold
Carlinhos atakosa mechi tatu zinazofuata akianza na mchezo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa mkoani Tanga March 04
Yanga ilihitaji kushinda mchezo huo ili kutinga raundi ya tano, Wananchi wamekamilisha mpango huo