Uongozi wa Yanga uko mbioni kufanya tathmini ya mali zake zote inazomiliki kabla ya kuanza mchakato wa mabadiliko.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wahabari Makao Makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam leo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema licha kuwa na mali zinazohamishika, klabu inamiliki mali nyingine zisizohamishika kama ardhi na Jengo lake.
Mkwasa amesema klabu itawasiliana na wataalamu wa tathmini za mali ili kuweza kutekeleza zoezi hilo.
"Tuna asset ambazo hazitembei kwa maana kama ardhi, sasa ni lazima tutafute thamani halisi ya ardhi tuliyonayo ili tuweze kubaini klabu yetu ina thamani kiasi gani," amesema Mkwasa.
"Siku chache zilizopita kuna klabu moja ilijitathmini kuwa ina thamani ya Bil 20 sasa sijui ni kwa vigezo gani lakini sisi kama mnakumbuka tunamiliki ardhi mtaa wa Mafya, pia tuna asset hapa klabu ambayo ni Jengo "
"Sasa tumepewa maelekezo tutafute watu wanaofanya uthamini wa mali ili tuweze kufahamu klabu yetu ina thamani gani."
Hivi karibuni mfanyabishara Mohammedi Dewji alishinda tenda ya uendeshaji wa klabu ya Simba yenye thamani ya Bil 20 ambapo sasa anamiliki hisa katika kampuni ya Simba Sport Club kwa asilimia 51.
Yanga imekusudia kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji kwa weledi zaidi.
Maamuzi ya kuanza mchakato wa mabadiliko yamefikiwa juzi Disemba 13 ambapo wajumbe wa Kamati ya utendaji walikutana kwenye kikao cha dharura.
Mkwasa amesema kulingana na Katiba ya Yanga ya mwaka 2010, Ibara 56 kipengele cha 3 kinajieleza kuwa wanachama wanatakiwa kumiliki hisa 51 na 49 inayobaki inaweza kwenda kwa Mwekezaji.
"Kikao hicho halali cha Kamati ya Utendaji kiliridhia na kupitia klabu kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko kwani kwa sasa ni lazima kuendesha klabu kwa mfumo unaokwenda na wakati," alisema Mkwassa.
Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga atatangaza mchakato mzima wa kuanza kwa mfumo huo baada ya zoezi la kuthamini mali za Yanga kukamilika.

ADVERTISE HERE