Waziri hajakata tamaa vita ya namba Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Feb 2021
Waziri hajakata tamaa vita ya namba Yanga

Mshambuliaji wa Yanga Waziri Junior amesema amejipanga kuhakikisha anapata nafasi kwenye kikosi cha kocha Cedric Kaze katika duru hii ya pili ligi kuu ya Vodacom

Waziri alitua Yanga mwanzoni mwa msimu baada ya kufanya vizuri katika kikosi cha Mbao Fc msimu uliopita, akiibuka kuwa mfungaji bora wa timu hiyo akiweka kambani mabao 16 katika mashindano yote

Hata hivyo ndani ya kikosi cha Yanga amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza licha ya kuwa ameifungia Yanga bao moja kwenye ligi

"Kila kitu kinawezekana, nasubiri wakati wangu utafika. Kama timu tuna ushirikiano mzuri ndio maana tuko juu kwenye msimamo wa ligi"

"Ningeweza kuondoka Yanga wakati wa dirisha dogo, lakini Mwalimu (Kaze) aliniambia nisiondoke kwa sababu anaamini nitakuwa na nafasi kwenye kikosi chake"

"Jukumu langu ni kuhakikisha napambana ili nikipewa hiyo nafasi niweze kuitumia vizuri," alisema Waziri

Kesho Jumamosi, Yanga itashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuikabili Kengold ukiwa ni mchezo wa raundi ya nne michuano ya kombe la FA

Huenda Waziri akapewa nafasi kwenye mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’