TFF itasikiliza malalamiko ya Yanga?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Feb 2021
TFF itasikiliza malalamiko ya Yanga?

Hivi karibuni Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredric Mwakalebela alitoa malalamiko mbalimbali akilituhumu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoitendea haki klabu hiyo katika masuala mbalimbali

Miongoni mwa tuhuma alizozitoa Mwakalebela kwa TFF ni chombo hicho chenye mamlaka ya usimamizi wa soka nchini kutojibu wala kusikiliza malalamiko ya Yanga juu ya kesi mbalimbali

Miongoni mwa kesi hizo ni ile ya Bernard Morrison ambapo Mwakalebela alibainisha kuwa waliiandikia barua TFF wakitaka mchezaji huyo azuiwe kuitumikia klabu ya Simba kwa kuwa mkataba wake haukuwa halali

Aidha Mwakalebela pia alibainisha kuwa Morrison hakurejesha fedha alizochukua Yanga pamoja na kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilimwamuri arudishe fedha zote

Mwakalebela alibainisha kuwa waliwasiliana na TFF kuhusu hatma ya fedha hizo lakini hawakupata majibu yoyote

Lakini pia, wakati TFF ikiwa haijasikiliza malalamiko yao, kupitia Kamati yake ya Maadili,ilisikiliza shauri lililomuhusu Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli na kumfungia kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitatu akidaiwa kuchelewa kulipa faini ya Tsh Milioni Tano kwa shauri lililokuwa likihusiana na kesi ya Morrison

Pia kulikuwa na suala la waamuzi ambao hawakuwa wakiitendea haki Yanga katika baadhi ya michezo na kupelekea mashabiki wa Yanga kufanya vurugu ambazo zinapelekea timu hiyo kuadhibiwa kila mara ya kamati ya Saa 72

Sasa TFF imeeleza kuwa tayari kusikiliza shutuma zilizotolewa wakiitaka klabu ya Yanga kuthibitisha shutuma hizo

"Baada ya kupitia shutuma zote, kamati imeona kuna haja ya mtoa shutuma kupewa haki ya msingi ya kusikilizwa na kuthibitisha madai yake mbele ya Kamati husika," ilisomeka sehemu ya taarifa ya Kamati

Kamati ya Usimamizi wa ligi imerejesha shauri hilo TFF ili lifikishwe mbele ya kamati inayohusika kwa ajili ya kusikilizwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13m ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’