Kamati ya Utendaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 24 2021, ilipitia mwenendo wa matukio mbalimbali ya Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza
Pamoja na maamuzi mengine, kamati hiyo imeitaka klabu ya Yanga itoe maelezo kwa nini isichukuliwe hatua kwa kosa la watu waliowapa majukumu ya ulinzi (mabaunsa) katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kuwafanyia vurugu wachezaji wa klabu ya Mtibwa Sugar kwenye njia ya kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo
Aidha klabu ya Mtibwa Sugar imetakiwa kuwaonya wachezaji wake kuhusu kujihusisha na vurugu. Hii ni kutokana na wachezaji wake kuonekana wakishiriki kwenye vurugu na mashabiki wa timu ya Yanga katika mchezo uliopigwa Februari 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa