Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Yanga keshokutwa Jumamosi watashuka uwanja wa Uhuru kumenyana na Kengold katika mchezo wa kombe la FA (ASFC), raundi ya tano
Huu ni mchezo ambao Yanga inahitaji kuondoka na ushindi ili kusonga mbele raundi ya tano ya michuano hiyo inayoendeshwa kwa utaratibu wa mtoano
Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi dimba la Uhuru kuiunga mkono timu yao
Viingilio vya mchezo huo Mzunguuko ni Tsh 5,000/- wakati VIP A na B ni Tsh 10,000/-
Ni Jumamosi hii pale uwanja wa Uhuru kuanzia saa kumi Alasiri
ADVERTISE HERE