Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mapinduzi Balama mwanzoni mwa mwezi ujao anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi akiwa mbioni kurejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa miezi tisa
Fundi huyo wa mpira alifanyiwa upasuaji mara mbili kutibu jeraha la kifundo cha mguu alilopata mwezi Juni 2020
Alitibiwa kwa mara ya kwanza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili lakini mwezi uliopita alilazimika kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi baada kubaini jeraha lake halikuwa limepona vizuri
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema Balama anatarajiwa kuanza mazoezi mwanzoni mwa mwezi wa tatu na atakuwa tayari kurejea kikosini baada ya wiki chache zaidi
Pengine Wananchi watamshuhudia Balama dimbani katika mechi za mwishoni mwa msimu huu
ADVERTISE HERE