Akiwa ameshuka dimbani mara 17, Deus Kaseke ndiye kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga akiwa amehusika kwenye mabao 10
Mabao yake sita aliyofunga na pasi nne za mabao, zinamfanya awe amehusika katika mabao 10
Ukitazama takwimu, unaweza kusema Kaseke ndiye mchezaji bora wa Yanga mpaka sasa
Amefunga mabao muhimu katika zile nyakati ambazo timu ilikuwa imepoteza matumaini
Kuna nyakati amekumbana na ukosoaji mwingi kutoka kwa mashabiki, pengine nao umeongeza kumuimarisha
Benchi la ufundi chini ya kocha Cedric Kaze pia wanastahili pongezi kwa ubora wa Kaseke
Tangu atue Yanga, Kaze ameonyesha kumuamini Kaseke hata zile nyakati ambazo mashabiki hawakutamani kumuona uwanjani
Lakini sasa ni wazi jina la Kaseke linapokuwemo katika orodha ya wachezaji wanaonza kikosini, mashabiki wanafarijika kwani wanajua muda wowote Kaseke anaweza kuwapa furaha