Nani anaikumbuka Yanga hii?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Feb 2021
Nani anaikumbuka Yanga hii?

Mwanzoni mwa mwezi March Mwaka 2014 wakati huo Al Ahly wakiwa mabingwa watetezi wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, walikuja nchini kucheza na Yanga raundi ya kwanza ya michuano hiyo

Ulikuwa mchezo ambao Nadir Haroub Cannavaro aliwatoa kimasomaso wananchi kwa kufunga bao pekee lililoihakikishia Yanga ushindi wa bao 1-0

Cannavaro aliweka bao hilo kambani kwenye dakika ya 83 akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Saimon Msuva

Lakini pia Wananchi hawakuishia hapo, walikwenda kuonyesha kandanda safi kule Misri pamoja na kuwa walikubali kipigo cha bao 1-0 na kulazimisha mchezo kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya matokeo ya jumla kuwa sare ya bao 1-1

Ulikuwa mchezo ambao Yanga walikaribia kuwaondosha mabingwa hao watetezi katika michuano ya ligi ya mabingwa kama sio penati ya Said Bahanuzi kupaa juu ya lango

Deo Munish wakati huo akiwa mlinda lango wa Yanga, alikuwa 'onfire' akiokoa penati mbili

Nadir Haroub, Didier Kavumbagu na Emmanuel Okwi walifunga mikwaju yao ya penati wakati Oscar Joshua aligongesha mwamba, Said Bahanuzi akapiga nje huku mkwaju wa Mbuyu Twite ukiokolewa na mlinda lango wa Al Ahly

Katika mchezo huo Yanga iliwakilishwa na kikosi hiki;

1.Dida, 2.Twite, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondani, 6.Domayo, 7.Msuva, 8.Ngasa/Chuji, 9.DKavumbagu, 10.Okwi, 11.Kizza/Bahanuzi

Kwa wale wasiofahamu, hawa Al Ahly sio mara ya kwanza kuja Tanzania na mara zote wamepigwa kikiwemo kipigo dhidi ya Yanga

Hata wakati huo wanapigwa na Yanga walikuwa ni mabingwa watetezi wa michuano ya ligi ya mabingwa ambayo walishinda mara mbili mfululizo msimu wa 2011/12 na 2012/13

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’