Jumamosi ya wiki hii, Februari 27 Yanga watashuka uwanjani kucheza mechi ya kwanza ya kombe la FA dhidi ya Kengold Fc ukiwa ni mchezo wa raundi ya tano
Vinara hao wa ligi kuu hawakucheza raundi iliyopita baada ya wapinzani wao Singida United kuondoshwa kwenye michuano hiyo
Singida United walishushwa madaraja mawili baada ya kushindwa kutokea uwanjani katika michezo miwili ya ligi daraja la kwanza
Mchezo kati ya Yanga dhidi ya Kengold utapigwa katika uwanja wa Uhuru, saa kumi jioni
Msimu huu wananchi wana jambo lao, wakipania kushinda kila taji la michuano wanayoshiriki
Walianza kwa kushinda kombe la Mapinduzi, wanalitaka hili la FA na muhimu zaidi ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom ambao utawahakikishia kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao
Wananchi wanasema hawahitaji kubebwa na timu yoyote kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao, watapambana wenyewe kupata tiketi