Namuunga mkono Shikhalo afanye vizuri - Metacha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2021
Namuunga mkono Shikhalo afanye vizuri - Metacha

Mlinda lango wa Yanga Metacha Mnata amesema anamungu mkono mlinda lango mwenzake Farouk Shikhalo anapopewa nafasi ya kucheza

Juzi Shikhalo alicheza mchezo wake wa pili kwenye ligi msimu huu, akipata cleansheet yake ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar

Metacha amesema Shikhalo amekuwa akimuunga mkono wakati wote anaocheza hivyo naye atafanya hivyo

"Nimefurahi yeye kuanza na nitamuunga mkono ili afanye vizuri. Siku zote ambazo mimi huwa nacheza naye ananiunga mkono sana, sote tunafanya kazi moja ya kuipigania timu," amesema Metacha

Baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze alisema kuwa katika duru ya pili anakusudia kumpa nafasi Shikhalo

"Metacha amecheza mechi nyingi katika duru ya kwanza, wakati huu tutampa nafasi zaidi Shikhalo pamoja na kuwa tutaendelea kumtumia kwenye FA," alisema Kaze

Shikhalo alirejesha imani ya mabosi wake kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar mwezi uliopita Yanga ikifanikiwa kushinda taji hilo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’