Kaseke kinara mabao Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2021
Kaseke kinara mabao Yanga

Deus Kaseke ndio kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga akiwa amefunga mabao sita

Michael Sarpong, Lamine Moro na Yacouba Songne nao hawako mbali nae wakiwa wameweka kambani mabao manne kila mmoja

Lakini pia Mukoko Tomombe, Carlinhos na Tuisila Kisinda nao wamefunga mabao matatu huku Saido Ntibazonkiza akiwa ameweka kambani mabao mawili

Wachezaji waliofunga bao moja mojo ni Waziri Junior, Bakari Mwamnyeto, Feisal Salum na Haruna Niyonzima

Pamoja na kufunga mabao sita, Kaseke pia ametoa pasi tatu za mabao hivyo kumfanya ahusike katika mabao tisa

Anayemfuatia ni Yacouba aliyehusika kwenye mabao nane (kafunga manne, asisti nne)

Tuisila yeye amehusika katika mabao saba, ana pasi nne za mabao na wakati akiwa aemfunga mabao matatu

Sarpong yeye amehusika katika jumla ya mabao sita kwani pamoja na mabao yake manne aliyofunga, ametoa pasi mbili za mabao

Lamine Moro, Saido Ntibazonkiza, Carlihos na Mukoko wao wamehusika katika mabao matano kila mmoja

Saido amefunga mawili na pasi tatu za mabao wakati Mukoko na Carlinhos wamefunga matatu na pasi mbili za mabao huku nahodha Lamine Moro akiwa na pasi moja na mabao manne

Wachezaji wengine waliohusika katika mabao ya Yanga pamoja na kuwa hawajafunga ni Farid Mussa (3), Ditram Nchimbi (2) na Kibwana Shomari (1)

Yanga imefunga jumla ya mabao 34 na kuruhusu mabao 11, Deus Kaseke akiwa mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi katika kikosi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’