Kaze bado ana imani na Sarpong

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2021
Kaze bado ana imani na Sarpong

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema ana imani na mshambuliaji Michael Sarpong licha ya nyota huyo kutokuwa na kasi nzuri ya kufunga mabao

Kaze amesema wengi hawafahamu kuwa kazi ya mshambuliaji sio kufunga tu, anapaswa kuwa sehemu ya timu na wakati mwingine inatosha kuwatengenezea wengine wakafunga

"Watu wanajidanganya sana, mshambuliaji sio kwamba anatakiwa kufunga magoli mengi. Mshambuliaji anaweza kufanya kazi ya kusaidia watu wengine kufunga"

"Ndio maana hadi leo nina imani na Sarpong kwa sababu anasaidia wenzake kufunga"

"Tunajua anaweza akafunga na itamsaidia kuongeza kujiamini kwenye mechi nyingine," amesema Kaze

Katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Sarpong alitoa pasi moja ya bao lililofungwa n Deus Kaseke licha ya kuwa yeye mwenyewe hakufunga kwenye mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 3-3

Wakati mwingine mikimbio yake imekuwa na faida kwa timu. Sarpong pia amejipambanua kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira

Hata hivyo ukubwa wa umbile lake wakati mwingine umemponza mbele ya waamuzi kwa kunyimwa adhabu pale anapofanyiwa madhambi na walinzi wa timu pinzani

Tangu atue Yanga mwanzoni mwa msimu huu, Sarpong amefunga jumla ya mabao sita, manne katika ligi kuu na mawili katika michezo ya kirafiki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’