Nyota Saido Ntibazonkiza na Yacouba Songne wako tayari kurejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua
Mafundi hao wameshaanza mazoezi na wenzao yakiwa ni maandalizi ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Kengold utakaopigwa wiki ijayo, Februari 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni kuwa Yacouba na Saido watakuwa tayari kuanza kuitumikia Yanga baada ya mchezo huo wa FA, kwa sasa wanajifua kurejesha 'fitness'
Kwa maana kwamba watakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri mkoani Tanga na Kilimanjaro kwa ajili ya mechi dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania ambazo zitapigwa March 04 na March 07
Yanga itacheza mechi hizo mbili mwezi March kabla ya ligi kusimama kupisha kalenda ya mechi za kufuzu fainali za Afcon 2022 Tanzania ikitarajiwa kucheza na Libya na Guinea Bissau