Wananchi wametakata uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Carlos Carlinhos ameibeba Yanga leo akifunga bao pekee la ushindi katika dakika ya 72
Carlinhos aliunganisha kimiani krosi mahiri iliyopigwa na Tuisila Kisinda 'Tk Master' aliyeambaa wingi ya kulia



Ulikuwa mchezo wenye upinzani mkali Mtibwa Sugar wakijilinda zaidi na kufanya mashambulizi kwa kushitukiza
Kipindi cha kwanza safu ya ushambuliaji ilikosa ubunifu wa kuipenya ngome ya Mtibwa Sugar lakini mabadiliko aliyofanya Kaze kwa kuwaingiza Carlinhos na Fiston Abdul Razak yaliinufaisha Yanga kwani katika kipindi cha pili nafasi nyingi zilitengenezwa
Wananchi leo walihitaji alama tatu, muhimu zaidi alama hizo zimepatikana na bila shaka ushindi huu utapunguza presha kwa wachezaji