Jana uongozi wa klabu ya Yanga ulizungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi kusikia upande wao juu ya nini kimewakwamisha kupata ushindi katika michezo miwili ya ligi kuu iliyopita dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar
Kilikuwa kikao cha ndani ambacho kilishirikisha uongozi wa juu, Kamati ya Utendaji chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla pamoja na wadhamini GSM, Injinia Hersi Said akishiriki kikao hicho kilichofanyika kule Avic Town, Mji ambao kambi ya Yanga ipo
Injinia Hersi amesema wamewasikia wachezaji, wamebaini maeneo ambayo yalikuwa na shida

Aidha kwa zile changamoto za kiufundi, benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Cedric Kaze, wamepewa maagizo ya kuhakikisha wanazitatua
"Kuna mambo ambayo ni ya ndani kama klabu, lakini niseme kuna upepo mbaya ulikuwa unapita"
"Tumezungumza na timu nzima, tumejua wapi kulikuwa na shida. Yote ya kuyafanyia kazi tumewaachia makocha kwa kuwa yako chini yao"
"Mashabiki wetu niwaombe kwamba hata sisi viongozi tumeumia kwa matokeo haya lakini tunaamini sasa tunarudi tukiwa imara kuanzia mchezo wa Jumamosi ," amesema Injinia Hersi
"Inawezekana yapo mengi ambayo ni ya kiufundi, ndio maana nasema tunawaachia makocha yale ambayo yanahitajika kufanyiwa kazi kama uongozi tutayafanyia kazi na hakuna shida ya kiutawala kwa maana ya wachezaji kukosa chochote wanachohitaji"
"Kama viongozi au wadhamini tumekuwa tukitimiza karibu kila kitu kwao, tuwaachie wao kwa kuwa wameahidi kurejea na nguvu kubwa"