Mshambuliaji Fiston Abdul Razak hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichoikabili Kagera Sugar juzi katika mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 3-3
Baadhi ya mashabiki walihoji kukosekana kwa mshambuliaji huyo lakini Kocha Cedric Kaze alikuwa na mipango yake
Ulikuwa mchezo ambao Kaze aliamua kumpumzisha nyota huyo raia wa Burundi ili aweze kujipanga
Fiston ameitumikia Yanga katika michezo miwili, mmoja ukiwa wa kirafiki dhidi ya African Sports na mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City
Katika michezo hiyo Fiston hakuonyesha makali yake, lakini ni mapema sana kumhukumu
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema mashabiki watarajie kumuone Fiston akiwa bora zaidi katika michezo ijayo
"Huyu ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Burundi, kinachomsumbua sasa ni changamoto ya ugeni ambayo huwakumba wachezaji wengi"
"Anachohitaji ni kuungwa mkono na mashabiki jambo ambalo litamfanya aongeze kujiamini na mchango wake kuweza kuonekana kikosini"