Kukosekana kwa kiungo Mukoko Tonombe katika kipindi cha kwanza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, kulipelekea Yanga kupoteana eneo la kiungo na kuwapa nafasi Kagera Sugar kutawala
Wengi wanaamini kukosekana kwa nyota huyo ilikuwa moja ya sababu iliyopelekea udhaifu katika safu ya ulinzi
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze alitaja sababu ya kutomtumia Mukoko katika kipindi cha kwanza kuwa alimpumzisha baada ya kucheza mechi mfululizo
Hata hivyo ni wazi Kaze alijutia uamuzi huo kwani timu yake iliyumba
Alipompa nafasi katika kipindi cha pili, Mukoko aliimarisha eneo la kiungo na kuirejesha Yanga mchezoni kwa kufunga bao safi la kusawazisha
Hizi mechi za duru ya pili ni sawa na vita hivyo unapaswa kutumia silaha zako zote kuweza kumshinda adui yako
Nizar Khalfan, kocha msaidizi wa Yanga anapaswa kumsaidia Kaze kufahamu ugumu wa mechi hizi