Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa leo Ijumaa saa 05:59 usiku ambapo mpaka sasa Yanga imethibitisha kusajili wachezaji wawili tu.
Mlinzi Fiston Kayembe amemalizia nafasi moja ya Kimataifa iliyokuwa imebaki huku Yohana Mkomola akiongezwa kwenye safu ya ushambuliaji.
Lakini habari njema ni kwamba mshambuliaji Amissi Tambwe ambaye alikuwa majeruhi kwa zaidi ya miezi minne naye amerejea kikosi hivyo kuimarisha zaidi safu ya ushambuliaji.
Aidha, baada ya kumalizana na uongozi, Donald Ngoma nae anarejea kuongeza zaidi ushindani katika safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa ikiwategemea wachezaji wawili Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa.
Thabani Kamusoko ndiye mchezaji pekee ambaye ni majeruhi na bado haijafahamika anarejea lini dimbani huku Kelvin Yondani aliyeumia kwenye michuano ya Chalenji nchini Kenya akitarajiwa kurejea dimbani wiki ijayo.
Kama Tambwe na Ngoma hawatakumbwa tena na majeraha ya kuwaweka nje kwa muda mrefu, bado Yanga itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne.
Yanga imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi lakini ikiwa inafunga mabao machache. Kurejea kwa Tambwe ni habari njema sana.
Wengi tulitamani kuona safu ya ushambuliaji inaongezwa nguzu zaidi kwa kusajili mshambuliaji wa Kimataifa, lakini ni vyema sasa tukaweka imani kwa hawa waliopo na benchi la ufundi.

ADVERTISE HERE