Sawa, ipo changamoto kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga kwa kushindwa kuzitumia nafasi nyingi wanazotengeneza
Lakini kwa hakika hili la makosa yanayofanywa na waamuzi katika michezo ya Yanga halipaswi kufumbiwa macho
Katika mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar Yanga ilistahili kupewa mikwaju mitatu ya penati, waliambulia mmoja
Hivi kwa nini mwamuzi hakutoa penati ile ya dakika za majeruhi? Kwani dhahiri shahiri mkono wa mlinzi wa Kagera Sugar ulizuia mpira wa Niyonzima ambao ulikuwa ukielekea wavuni
Tukio lile lina tofauti gani na tukio la mkwaju wa penalti ambao Mbeya City walipewa kule mkoani Mbeya?
Hatukatai, Yanga wanapaswa kufanyia kazi changamoto kwenye safu ya ushambuliaji lakini hilo halitoi uhalali kuwaonea pale wanapostahili haki
Wachezaji wanapambana sana, kuendelea kwa matukio haya kunawakatisha tamaa