Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kesho Jumatano uwanja wa Benjamin Mkapa wakati timu yao itakaposhuka dimbani kuikabili Kagera Sugar
Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City, Yanga imepania kusahihisha makosa kwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo
"Tumefanya maandalizi ya kutosha, naweza kusema vijana wako tayari kwa mchezo. Tunafahamu ugumu wa mchezo huo lakini tunawahakikisha mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani, tutapambana kuhakikisha tunapata ushindi," amesema Meneja wa Yanga Hafidh Saleh
Yanga imeweka hadharani viingilio vya mchezo huo ambapo Mzunguuko ni Tsh 5,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na VIP A ni Tsh 15,000/-. Mchezo utapigwa kuanzia saa moja kamiliΒ usiku
Mtanange ni kama fainali kwa Yanga kwani Wananchi wanahitaji kuondoka na alama zote tatu ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi
Ikumbukwe wako katika ushindani mkali kwenye mbio za ubingwa na watani zao Simba ambao wana viporo viwili mkononi na watashuka dimbani keshokutwa Alhamisi kuikabili Biashara United wilayani Musoma