Timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes' leo wanatupa karata yao ya kwanza kwenye michuano ya AFCON U20 inayofanyika nchini Mauritania kwa kuikabili Ghana
Mchezo huo wa kwanza kundi C, utapigwa kuanzia saa moja usiku kwa saa za Tanzania na utarushwa mbashara na ZBC 2 kupitia kisimbuzi cha Azam
Ngorongoro Heroes wako kundi C pamoja na timu za Morocco, Ghana na Gambia
Kundi hili linatazamwa kama kundi la kifo kwa kuzijumuisha pamoja Morocco na Ghana
Kila la kheri Ngorongoro Heroes
ADVERTISE HERE