Ukifuatilia baadhi ya redio na mitandao ya kijamii utaona imeanza kutengenezwa mijadala yenye lengo la kuvuruga utulivu uliopo ndani ya Yanga hasa baada ya matokeo ya mchezo dhidi ya Mbeya City
Mijadala mingi inaanzishwa na watu ambao hawana nia nzuri na Yanga. Siamini kama kuna mshabiki wa Yanga anaweza kutoka hadharani kumnyooshea kidole kocha Cedric Kaze na wachezaji wake eti sababu timu imelazimishwa sare dhidi ya Mbeya City!
Kila mmoja aliona juhudi ambazo wachezaji walionyesha katika mchezo huo, pamoja na changamoto zilizojitokeza
Muhimu zaidi, Wanayanga wa kweli wanafahamu timu yao ilipotoka, ilipo na inapoelekea
Mpaka sasa Yanga ndio klabu yenye msimu bora, iko kileleni mwa msimamo wa ligi lakini pia haijapoteza mchezo
Ni mwezi uliopita tu Kaze ameipa Yanga taji lake la kwanza baada ya misimu mitatu bila ya kushangilia taji
Wanayanga hatupaswi kusikiliza kelele zao kwani hazina nia nzuri, tujikite katika kuiunga mkono timu yetu ili tuweze kufikia malengo
Jumatano kuna mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Wananchi tuweke malengo yetu huko kuhakikisha tunashinda mchezo huo