Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtangaza Kim Poulsen raia wa Denmark kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
Taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, imebainisha kuwa Poulsen amesaini mkataba wa miaka mitatu
Kibarua chake cha kwanza ni kusaka nafasi ya kutinga fainali za Afcon 2022 na kombe la dunia michuano itakayofanyika kule Qatar
Poulsen aliwahi kuinoa Stars mwaka 2012 na 2013 akipewa majukumu haya baada ya kupata mafanikio wakati akiinoa timu ya Taifa ya vijana
Poulsen amechukua nafasi iliyoachwa na Etienne Ndayiragije ambaye hivi karibuni TFF ilitangaza kufikia nae makubaliano ya kuvunja mkataba wake

ADVERTISE HERE