Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza ataendelea kuwa nje kwa wiki kadhaa zaidi baada ya kubainika kuwa na uvimbe kwenye maungio ya paja na kiuno
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema mshambuliaji huyo anaendelea kupewa tiba maalum ya mionzi
Muda ambao ataendelea kukosekana ni wiki nne au zaidi kutegemea na uponaji wa majeraha hayo
Saido anaweza kukosa michezo mitano akianza na mchezo dhidi ya Kagera Sugar February 17, dhidi ya Mtibwa Sugar February 20, dhidi ya Kengold Fc (ASFC) February 28, dhidi ya Coastal Union March 04 Ugenini, dhidi ya Polisi Tanzania March 07 ugenini
Hii sio habari nzuri sana kwa mashabiki wa Yanga ambao walitamani kumuona dimbani siku ya Jumatano wakati Yanga itakapoikabili Kagera Sugar
Lakini habari njema ni kurejea kikosini kwa mshambuliaji Yacouba Songne anayeweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Kagera Sugar