Mchezo wa ligi kuu kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga umemalizika kwa timu hizo kugawana alama baada ya kutoka sare ya bao 1-1
Deus Kaseke ndiye aliyeitanguliza Yanga kwa kuifungia bao kwenye dakika ya 84 bao ambalo mlinzi wa Mbeya City aliokoa mpira ukiwa tayari umevuka mstari
Hata hivyo haikuwa bahati kwa Yanga kwani kwenye dakika za majeruhi Mbeya City walipata mkwaju wa penati baada ya mpira kumgonga Yassin Mustafa katika mkono wake akiwa ndani ya eneo la hatari



Bado changamoto inaonekana katika umaliziaji kwani mwanzoni kabisa mwa mchezo, Yanga walitengeneza nafasi kadhaa ambazo hawakuweza kuzitumia
Yanga sasa inarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Februari 17 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE