Nani aanze, nani asubiri vs Mbeya City leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Feb 2021
Nani aanze, nani asubiri vs Mbeya City leo?

Jioni ya leo kikosi cha Yanga kitashuka kunako dimba la Sokoine kuikabili Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amethibitisha kuwa katika mchezo huo atawakosa wachezaji wake wawili Saido Ntibazonkiza na Yacouba Songne

Ntibazonkiza alibaki jijini Dar es salaam akiendelea kupona majeraha yanayomsumbua wakati Yacouba yuko na timu Mbeya lakini bado hajawa timamu kwa silimia 100

Ni mchezo ambao mshambuliaji mpya Fiston Abdul Razak atakuwa na nafasi ya kuanza katika mchezo wake wa kwanza kwenye ligi

Huu utakuwa mchezo ambao Fiston anaweza kuutumia kuwanyamazisha wakosoaji wake wanaosubiri kuona hafanikiwa katika ligi ya Tanzania

Pamoja na Fiston, washambuliaji Ditram Nchimbi, Waziri Junior na Michael Sarpong nao wako tayari kuwa na mchango wao katika mchezo huo

Nchimbi alikuwa mshambuliaji tegemeo kwenye kikosi cha Tanzania kilichoshiriki michuano ya CHAN iliyomalizika wiki iliyopita nchini Cameroon

Yeye pamoja na Farid Mussa walikuwa na mashindano mazuri. Bila shaka Kaze anaweza kuwaamini leo na kuwaanzisha katika kikosi chake

Safu ya ulinzi leo inatarajiwa kuwa kamili kwani Metacha, Kibwana, Yassin, Lamine na Mwamnyeto wote wako timamu wakisubiri kupute hicho

Carlinhos anatarajiwa kupewa majukumu yaliyokuwa yakifanywa na Ntibazonkiza wakati TK Master yeye yuko tayari kupima umri sahihi wa walinzi wa Mbeya City

'Mwaisa' Deus Kaseke ambaye ana msimu bora ndani ya kikosi cha Yanga, pia anaweza kuwa na nafasi yake katika mchezo huo

Wakati pale eneo la kiungo Mukoko Tomombe na Feisal Salum wote wapo timamu kuendeleza pale walipoishia kabla ya mapumziko ya CHAN

Hakuna wanachosubiri Wananchi zaidi ya kuishuhudia timu yao ikicheza kandanda safi litakaloambatana na ushindi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’