Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Etienne Ndayiragije
Taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, imebainisha kuwa wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa kocha huyo raia wa Burundi
"Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije," taarifa ya TFF imebainisha

Lilikuwa ni suala la muda kwa uamuzi huo kutangazwa kwani tayari TFF ilishaanza mchakato wa kusaka mbadala wake, kocha wa zamani ya timu ya vijana Kim Paulsen akiwa miongoni mwa makocha wanaotajwa kurithi mikoba yake
Ndayiragije hakupata uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka nchini kutokana na mbinu zake na hata uteuzi wa wachezaji