Keshokutwa Jumamosi Yanga itakuwa mkoani Mbeya pale uwanja wa Sokoine kuikabili Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Vinara hao wa ligi kuu wanatarajiwa kutua mkoani Mbeya mchana wa leo
Deus Kaseke nyota wa zamani wa Mbeya City , ni miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa katika msafara wa kikosi cha Yanga
Kaseke anatarajiwa kuwakabili waajiri wake hao wa zamani
Hapa tunamzungumzia mchezaji ambaye mwanzoni mwa msimu alikumbana sana na ukosoaji lakini imani iliyowekwa kwake na kocha Cedric Kaze matunda yake yameonekana
Ni miongoni mwa vinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga akiwa amefunga mabao manne sawa na Lamine Moro, Michael Sarpong na Yacouba Songne
Yeye na Songne wamekuwa na ushirikiano wa kipekee kwani katika mechi ambazo wawili hao wamecheza pamoja, walihusika kusababisha bao mmoja akitengeneza na mwingine kufunga

Kwa ara nyingine wanaweza kuwa pamoja kule Mbeya kwani Yacouba pia amejumuishwa katika kikosi baada ya kupona majeraha
Kaseke alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa kilichoshiriki michuano ya CHAN kule Cameroon
Wachezaji wengine waliokuwa kule Cameroon ni Feisal Salum, Yassin Mustafa, Bakari Nondo Mwamnyeto, Farid Mussa na Ditram Nchimbi
Nyota wote wamerejea kikosini na wanaelekea mkoani Mbeya kusaka alama tatu muhimu kwa ajili ya Yanga