Maandalizi ya kuiwinda St Louis yameaanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Dec 2017
Maandalizi ya kuiwinda St Louis yameaanza
Siku moja baada ya droo ya michuano ya ligi ya mabingwa kufanyika, uongozi wa Yanga umesema umeanza maandalizi kuelekea mchezo wao dhidi ya St Louis ya Shelisheli.

Yanga itachuana na St Louis, mabingwa wa Shelisheli kwenye mchezo wa hatua ya awali kusaka tiketi ya kutinga mzunguuko wa kwanza wa michuano hiyo.

Mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Februari 09-11, 2018 jijini Dar es Salaam na mchezo wa marudiano utafanyika wiki moja baadae huko Shelisheli.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema Yanga haiidharau St Louis na ndio maana imeanza mapema ya kuhakikisha inapata ushindi mnono kwenye mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Taifa.

"Baada ya ratiba kutoka moja kwa moja maandalizi yanaanza, tunacheza dhidi ya timu ya Seychelles huwezi kudharau timu, ni timu nzuri ndio maana imefika hapo ilipo kwa hiyo kila timu inahitaji kupambana ili kupata matokeo hakuna timu ya kubeza. Huwezi kusema hii inatoka kwenye nchi ndogo na ligi ambayo ni nyepesi," amesema Ten

"Kitu kizuri kwetu ni kwamba benchi la ufundi wameona ratiba wamefahamu timu ambayo tunaenda kucheza nayo kwa hiyo matayarisho yanaanza kuona kwamba tunaenda kufanya vizuri kuliko msimu uliopita."

Mshindi wa hatua ya awali atatinga mzunguuko wa kwanza ambapo atachuana na mshindi kati ya El Marreikh ya Sudani na Township Rollers ya Botswana.

Mshindi wa mzunguuko wa kwanza atatinga moja kwa moja hatua ya makundi ambayo ni 16 bora ya ligi ya mabingwa wakati timu itakayofungwa itashushwa kwenye michuano ya kombe la shirikisho mzunguuko wa pili.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’