Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kuachana na aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije pamoja na benchi lake lote la ufundi
Inaelezwa kocha wa zamani wa Stars ambaye alisimamia timu za vijana kwa mafanikio makubwa Kim Paulsen tayari yuko nchini kumalizana na TFF aweze kukabidhiwa mikoba
Mafanikio makubwa aliyopata Ndayiragije akiwa na Stars ni kushiriki fainali za michuano ya CHAN zilizamalizika hivi karibuni nchini Cameroon
Aidha Ndayiragije ameiongoza Tanzania kwenye mechi tatu za kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Afcon zijazo akishinda mchezo mmoja, sare moja na kufungwa mchezo mmoja
ADVERTISE HERE