Beki kisiki Abdallah Shaibu 'Ninja' hivi karibuni alikumbwa na changamoto ya kuugua Malaria
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema beki huyo aliyen'gara kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar mwezi uliopita, bado ni mgonjwa
"Ni kweli Ninja hajafanya mazoezi kwa siku kadhaa kwa sababu anasumbuliwa na malaria. Anaendelea na matibabu, ataungana nasi pale atakapopona," alisema
Aidha akizungumzia maandalizi ya kikosi kuelekea mchezo dhidi ya Mbeya City, Hafidh amesema wameendelea na program za mazoezi na wako tayari kusafiri kwenda Mbeya
"Jana na leo tumeendelea na mazoezI, ukimuondoa Saido Ntibazonkiza ambaye anasumbuliwa na nyama za paja, wachezaji wangine wameshiriki mazoezi vizuri"
Jana kocha Cedric Kaze alisema Ntibazonkiza ana asilimia 50 za kushiriki mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumamosi, Februari 13 uwanja wa Sokoine