Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amethibitisha kuwa mshambuliaji Michael Sarpong amepata majeraha ya goti yaliyomfanya akose mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports juzi
Sarpong ameungana na nyota wengine watatu wanaosumbuliwa na matatizo ya misuli na nyama za paja
Saido Ntibazonkiza, Yacouba Songne na Dickson Job wanasumbuliwa na matatizo ya misuli
Ntibazonkiza na Job tayari walishaanza mazoezi mepesi
Aidha mlinda lango Ramadhani Kabwili nae ni majeruhi akiwa anaendelea vizuri
Kikosi cha Yanga kinaendelea kujifua kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumamosi, Februari 13 mkoani Mbeya
ADVERTISE HERE