Mechi za ligi kuu ya Vodacom duru ya pili zinarejea wiki ijayo ambapo Yanga itaanzia kule mkoani Mbeya kuikabili Mbeya City katika mchezo ambao utapigwa Februari 13 uwanja wa Sokoine
Katika mwezi huu wa pili Yanga itacheza mechi tatu ambapo baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City, Wananchi watareje jijini Dar es salaam ambako watakuwa na mechi mbili nyumbani dhidi ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar
Mchezo dhidi ya Kagera Sugar utapigwa Februari 17 wakati mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utapigwa Februari 20
Wananchi wamepania kuendelea palepale walipoishia wakati ligi iliposimama kupisha michuano ya CHAN mwezi uliopita

ADVERTISE HERE