Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mapinduzi Balama rasmi amemkabidhi jezi namba saba mshambuliaji Fiston Abdul Razak
Fiston aliyetua Yanga katika usajili wa dirisha dogo, anatarajiwa kuanza kuivaa jezi hiyo leo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Balama ameeleza kuridhia Fiston kutumia jezi hiyo
"Nimeridhia kumkabidhi Fiston jezi namba saba, namtakia kila la kheri," aliandika Balama
Kiungo huyo bado anauguza kidonda baada ya hivi karibuni kufanyiwa upasuaji wa jeraha kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia
Anatarajiwa kurejea uwanjani mwezi ujao ambapo uongozi wa Yanga umesema nyota huyo atakabidhiwa jezi nyingine
Hongera Balama kwa kuwa muungwana...!
ADVERTISE HERE