Kutumia jezi ya Yanga kufanya matangazo binafsi tena kwa kuondoa jina la Mdhamini Mkuu kampuni ya Sportpesa sio jambo la kiungwana
Huu utani wa jadi sasa unatumika vibaya sana kwani wapo watu wamekuwa mahodari 'kujifichamo' humo wakitukana, kukashifu na kudharau brand za wengine
Hili tukio lililofanywa na Msemaji wa Simba Haji Manara ni mwendelezo wa matukio mengi tu ambayo amekuwa akiyafanya dhidi ya Yanga kwa kisingizio cha utani wa jadi

Katika nchi za wenzetu mambo kama haya huwezi kuyaona yakifanywa na kiongozi lakini huku kwetu tumeyaachia sana kiasi kwamba wapo wanaodhani wana uhuru wa kufanya jambo lolote wakijificha kwenye kichaka cha utani wa jadi
Naamini wadhamini GSM hawataliacha hili lipite hivihivi. Wao ndio watengenezaji na wasambazaji wa jezi za klabu ya Yanga
Na huyu aliyefanya tukio hili ni mmoja wa mabalozi wa kutangaza bidhaa zao!
Wanayanga wamechukizwa sana na kitendo kilichofanyika, wengi wanasubiri kuona ni hatua gani ambazo uongozi pia utachukua ili kukomesha matukio haya