Injinia awasiliana na Tambwe kukamilisha malipo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Feb 2021
Injinia awasiliana na Tambwe kukamilisha malipo

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amisi Tambwe amekiri kuwa jana aliwasiliana na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Saidi kwa ajili ya kukamilisha malipo ya fedha anazoidai klabu hiyo

Juzi baada ya kuibuka taarifa kuwa Yanga itazuiwa kufanya usajili kwa madirisha matatu kama haitamlipa mshambuliaji huyo kiasi cha Tsh Milioni 44 anazodai, uongozi wa Yanga ulikiri kupokea barua ya FIFA inayowaelekeza walipe deni hilo

Aidha Injinia Hersi kwa niaba ya GSM, alisema kuwa deni hilo litalipwa kabla ya siku ya leo Ijumaa kumalizika

"Ni kweli jana nilipigiwa simu na Injinia Hersi Said, kwa ajili ya kufanya mchakato wa malipo fedha ninazodai," alisema Tambwe

Kumekuwa na msululu wa wachezaji ambao wana madai Yanga, uongozi umeahidi kuendelea kulipa taratibu

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema waliweka utaratibu wa kulipa madeni hayo, wataendelea nao

Kati ya mwaka 2015 na 2019 Yanga ilikumbwa na changamoto kubwa ya kiuchumi hasa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wake Yusufu Manji kukumbwa na matatizo

Matatizo hayo yalipelekea Manji akajiuzulu nafasi zake zote za uongozi ndani ya Yanga, tukio ambalo kwa hakika liliiweka Yanga katika njia panda kwani yeye ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’