Mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndani ya klabu ya Yanga unaendelea ambapo hatua inayofuata ni rasimu ya Mabadiliko kuwasilishwa kwa Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ajili ya utambulisho.
Aidha Mshauri Mkuu wa mchakato huo, Senzo Mazingisa amesema kuwa Rasimu hiyo tayari imetafsiriwa kwa Kiswahili ili kueleweka kwa urahisi
Itawasilishwa kwa viongozi wote wa Matawi ya Yanga na kisha kufuatiwa na zoezi la kutoa elimu kwa Wanachama nchi nzima
"Mchakato wetu wa Mabadiliko unaendelea ambapo hatua tuliyopo tunaishirikisha Serikali kwa kuiwasilisha rasimu hiyo kwa ajili ya mapitio. Tunataka kufanya Mabadiliko ambayo yataridhiwa na Serikali na kuwa hayaendi kinyume na matakwa ya sheria za nchi"
"Baadae tutakutana na viongozi wa matawi nchi nzima, tutazunguuka kukutana na Wanachama na mashabiki kuhakikisha elimu husika inawafikia wote"