Wakati wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu ya Taifa wakimalizia siku za mapumziko waliyopewa, kiungo Deus Kaseke yeye ameripoti kambini mapema kuendelea na mazoezi na wachezaji wengine
Kaseke alikuwa kule Cameroon na Stars akipata nafasi ya kucheza mechi moja kati ya tatu ambazo Tanzania ilicheza
Katika kikosi cha Yanga, msimu huu Kaseke ameweka kambani mabao manne kwenye ligi pamoja na kutoa pasi mbili za mabao
Amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Kocha Cedric Kaze wakati mwingine akiongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji
ADVERTISE HERE