Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amesema mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Amisi Tambwe atalipwa fedha zake kwa utaratibu ambao Yanga wamekuwa wakiutumia kuwalipa wote wanaoidai klabu hiyo
Baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa Yanga imefungiwa kusajili kwa madirisha matatu mpaka pale itakapokamilisha kumlipa Tambwe fedha anazodai, Dk Msolla amesema Yanga italipa deni hilo
"Naomba ifahamike, tuna utaratibu wetu wa kulipa madeni, tumekuwa tukilipa kidogo kidogo hata FIFA wanafahamu. Ndio utaratibu tuliotumia kuwalipa waliokuwa makocha wetu George Lwandamina na Mwinyi Zahera"
"Hivyo niseme tu Tambwe nae atalipwa kwa utaratibu huo lakini siwezi kusema ni mpaka lini tutakuwa tumemalizana nae muhimu tu ifahamike kuwa tutamlipa," alisema
GSM kumaliza kila kitu kitu
Wakati Mwenyekiti Dk Msolla akiahidi kulipa deni hilo taratibu, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Mhandisi Hersi Said amesema hadi kufikia Ijumaa (kesho) watakuwa wameilipa fedha yote
Hersi amesema sakata hili lilijitokeza kabla ya ujio wao lakini wanawahakikishia Wananchama na Mashabiki wa Yanga kuwa watalimaliza, wapo imara na wamedhamiria kuijenga Yanga imara ndani na nje ya uwanja