Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amethibitisha kuwa wamepokea ofa kutoka klabu moja inayoshiriki ligi kuu nchini China ikimtaka mshambuliaji Michael Sarpong raia wa Ghana
Injinia Hersi amesema Yanga itanufaika na dili hiyo ya usajili itakapokamilika
Aidha amesema wale wanaombeza mshambuliaji huyo, hawataamini faida ambayo klabu ya Yanga itapata
"Sarpong amekuwa mhimili mkubwa wa safu yetu ya ushambuliaji lakini wapo watu wasiomtakia mema ambao wanambeza"
"Watu hao watashangazwa dili hilo likikamilika kwani Yanga itapata faida kubwa sana," alisema
Imeelezwa Yanga inaweza kuvuna kitita cha sio chini Tsh Bilioni Moja dili lake litakapokamilika huko Uchina
ADVERTISE HERE